FAQ · Maswali ya Kawaida

Una swali? Tuna jibu.

Maswali ya kawaida kuhusu delivery, malipo, na zaidi.
Got a question? We have you covered.

Delivery Megamart inadelivery wapi Dar es Salaam?
+

Megamart inadelivery katika maeneo yote ya Dar es Salaam ikiwemo Posta, Kariakoo, Kinondoni, Ilala, Temeke, Mbagala, Kijitonyama, na Mikocheni. Tunaanza na Posta area na tunaendelea kupanua maeneo zaidi kila wiki.

Delivery Delivery inachukua muda gani?
+

Ndani ya Posta area na maeneo ya karibu, delivery inachukua saa 1–3. Maeneo mengine ya Dar es Salaam inachukua saa 3–6 kulingana na umbali na msongamano wa magari.

Delivery Naweza kufuatilia order yangu?
+

Ndiyo. Megamart ina live rider tracking — utaona rider wako kwenye ramani wakati anaelekea kwako. Utapata ujumbe wa SMS/WhatsApp ukithibitisha order na wakati wa delivery.

Malipo Ninaweza kulipa vipi?
+

Megamart inakubali M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, na Cash on Delivery (lipa pale unapopokea bidhaa). Hakuna ada ya ziada kwa njia yoyote ya malipo.

Malipo Je, kuna bei ya chini ya order?
+

Hapana bei ya chini ya lazima. Unaweza kuorder bidhaa moja au nyingi unavyotaka. Ada ya delivery inategemea umbali wa eneo lako.

Bidhaa Megamart ina bidhaa gani?
+

Megamart ina bidhaa za nyumbani, electronics, groceries, fashion, na zaidi. Orodha ya bidhaa inaendelea kukua. Unaweza kutafuta bidhaa yoyote kwenye app au website yetu.

Bidhaa Bidhaa zote ni halisi (genuine)?
+

Ndiyo. Megamart inauza bidhaa halisi tu kupitia wasambazaji walioidhinishwa. Kila bidhaa inakaguliwa kabla ya kutumwa kwako.

Returns Nikitaka kurudisha bidhaa nifanye nini?
+

Ukipokea bidhaa iliyoharibika au si ile uliyoorder, wasiliana nasi ndani ya saa 24 kupitia WhatsApp au simu. Tutarekebisha mara moja bila malipo ya ziada.

Bado una swali?

Timu yetu iko tayari kukusaidia kupitia WhatsApp au simu.